Genesis 26:15-22

15 aKwa hiyo visima vyote vilivyochimbwa na watumishi wakati wa Abrahamu baba yake, Wafilisti wakavifukia, wakavijaza udongo.

16Ndipo Abimeleki akamwambia Isaki, “Ondoka kwetu, kwa maana umetuzidi nguvu sana.”

17Basi Isaki akatoka huko akajenga kambi katika Bonde la Gerari, akaishi huko. 18Ndipo Isaki akavichimbua tena vile visima vya maji ambavyo vilichimbwa siku zile za Abrahamu baba yake, ambavyo Wafilisti walivifukia baada ya kufa Abrahamu, akavipa majina yale yale ambayo baba yake alikuwa amevipa.

19Watumishi wa Isaki wakachimba katika lile bonde wakagundua huko kisima chenye maji safi. 20Lakini wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaki wakisema, “Maji haya ni yetu!” Ndipo akakiita kile kisima Eseki,
Eseki maana yake ni Ugomvi.
kwa sababu waligombana naye.
21Kisha wakachimba kisima kingine, lakini hata hicho pia wakakigombania, akakiita Sitna.
Sitna maana yake Upinzani.
22 dAkaondoka huko, akachimba kisima kingine, wala hakuna yeyote aliyekigombania. Akakiita Rehobothi,
Rehobothi maana yake ni Mungu ametufanyia nafasi.
akisema, “Sasa Bwana ametufanyia nafasi, nasi tutastawi katika nchi.”

Copyright information for SwhNEN